#Local News

IPOA YACHUNGUZA MAUAJI LUANDA

Mamlaka ya kitaifa inayoangazia utendakazi wa polisi IPOA, imeanzisha uchunguzi katika kifo cha mtu mmoja katika eneo la Luanda kaunti ya Vihiga polisi waliponasa pikipiki 20 zinazohusishwa na wizi.

Wakati wa tukio hilo la hivi majuzi, wakazi walipinga kunaswa kwa pikipiki hizo na kuifunga barabara kuu ya Kisumu-Busia na kusababisha ghasia, walipojaribu kuvamia kituo cha polisi ili kuchukua pikipiki zao.

IPOA wanachunguza kubaini iwapo hatua ya polisi kunasa pikipiki hizo ilikuwa halali au la, katika tukio ambalo pia liliwaacha polisi sab ana majeraha.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *