KCCPS YAFUNGA MFUMO WA KUTUMA MAOMBI
Zoezi la wanafunzi waliofanya mtihani wa KCSE mwaka jana kutuma maombi ya kusajiliwa katika vyuo vikuu nchini kupitia KUCCPS limefungwa rasmi usiku wa kuamkia leo, ikibainika kuwa idadi kubwa ya wanafunzi walichagua kozi mbali mbali ila hawakukamilisha mchakato wa kutuma maombi yao.
Afisa mkuu mtendaji wa KUCCPS Dr. Mercy Wahome, ameweka wazi kwamba kuchagua kozi pekee hakutoshi iwapo mwanafunzi hatabonyeza kitufe cha mwisho ili kuwasilisha maombi na kuzingatiwa katika awamu ya kwanza.
Kulingana na taasisi hizo, zaidi ya nafasi milioni 1.4 zinapatikana katika vyuo vikuu na taasisi za mafunzo ya kiufundi nchini.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 














































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































