#Local News

RUTO AZINDUA KANGAMANO LA ELIMU NAIVASHA

Rais William Ruto amesisitiza mageuzi makubwa katika sekta ya elimu nchini, akieleza kuwa serikali inalenga kuhakikisha mfumo wa elimu unalenga ujuzi, ubunifu na mahitaji ya soko la ajira.

Katika hotuba yake mjini Naivasha Ruto ametaja umuhimu wa taifa kueka  mkazo kwenye ubora wa ufundishaji na mazingira bora ya kujifunzia ili kuinua viwango vya kitaaluma kwa wanafunzi wote nchini

Ameahidi kuwa serikali itaongeza uwekezaji katika miundombinu ya shule, mafunzo kwa walimu na matumizi ya teknolojia katika elimu ili kuendana na mabadiliko ya dunia ya sasa.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *