VIONGOZI TRANS NZOIA WALALAMIKIA ‘MSAKO WA KISIASA’
Huku kikosi maalum cha polisi kikiendeleza msako dhidi ya magenge ya wahalifu katika kaunti ya Trans Nzoia, imeibuka kwamba operesheni hiyo inakiuka haki za kimsingi za raia.
Akizungumza na wanahabari baada ya maafisa wake wakuu 2 kukamatwa kwa kuhusishwa na uhalifu, gavana wa kaunti hiyo George Natembea, amesema operesheni hiyo imekiuka sheria na kuwalenga wakosoaji wa serikali.
Hata hivyo, naibu inspekta mkuu wa polisi Eliud Lagat ametetea msako huo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 














































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































