#Football #Sports

AFCON 2027: KENYA YATANGAZA VIWANJA VITAKAVYOTUMIKA

Viwanja vya Kasarani na Talanta Sports City unaoendelea kujengwa ndivyo vitakavyotumika katika mashindano ya kombe la mataifa bingwa barani Afrika, AFCON mwaka ujao, yatakayoandaliwa kwa pamoja katika mataifa ya Kenya, Uganda na Tanzania.

Haya ni kulingana na katibu mkuu katika wizara ya michezo Elijah Mwangi, akisema uwanja wa Nyayo umewekwa katika kategoria ya viwanja mbadala, na hatuatumika kama uwanja mkuu kwenye mashindano hayo.

Wakati uo huo, uwanja wa Ulinzi Sports Complex, Police Sacco Grounds, Moi International Sports Centre Annex 1 na Annex 2, Kenya Academy of Sports Grounds 1 na 2, Utalii College, Talanta Sports City Stadium 1 na Kirigiti Stadium vimetengwa kama viwanja vya kufanyia mazoezi.

Tangazo hilo linajiri baada ya shirikisho la soka barani Afrika, CAF, kutangaza tarehe kuu za mechi ya ufunguzi na fainali ya mashindano hayo ya AFCON.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *