#Local News

MUTULA AMKOSOA DUALE KUHUSU KAULI ZA NGAMIA

Gavana wa Makueni Mutula Kilonzo Jr amemkosoa Waziri wa Afya Aden Duale kufuatia matamshi yake kuhusu ngamia wanaotoka Garissa kuharibu mimea katika maeneo ya Ukambani.

Mutula amesema kauli hizo hazifai kutolewa na kiongozi wa kitaifa, hasa wakati ambapo kuna mvutano wa kiusalama katika eneo la Mwingi kati ya wafugaji wa ngamia na wakulima.

Amesisitiza kuwa viongozi wanapaswa kutafuta suluhu ya amani na kulinda maslahi ya wananchi badala ya kutoa matamshi yanayoweza kuchochea migogoro zaidi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *