#Local News

RUTO AZINDUA KITUO CHA HUDUMA LAIKIPIA

Rais William Ruto amezuru Kaunti ya Laikipia ambapo amezindua mradi wa ujenzi wa kituo cha huduma katika eneo la Doldol ili kusogeza huduma za serikali karibu na wananchi.

Rais ameahidi kuwa ujenzi wa barabara ya kilomita 60 kutoka Nanyuki kuelekea Doldol utaanza ndani ya wiki mbili zijazo, akiongeza kuwa serikali yake itajenga kilomita 217 zaidi za barabara za lami katika kaunti hiyo.

Aidha, Ruto amewakosoa viongozi wa upinzani akisema wanaeneza siasa za upotoshaji badala ya kuwatumikia wananchi kupitia miradi ya maendeleo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *