AISHA JUMWA AONDOLEWA KAMA MWENYEKITI WA BODI YA BARABARA NCHINI (KRB)
Mahakama Kuu imeondoa uteuzi wa aliyekuwa Waziri wa Mawaziri Aisha Jumwa kama Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara za Kenya KRB, ikitoa uamuzi kwamba mchakato huo umekiuka Katiba na mahitaji ya kisheria.
Kulingana na Jaji Mwamuy aliyetoa hukumu hiyo ni kuwa uteuzi wa Jumwa umefanywa bila kuthibitishwa kufuata Kifungu cha 7 cha Sheria ya Bodi ya Barabara za Kenya na ni ukiukaji wa Vifungu vyenye nambari 10, 47 na 232 vya Katiba, vinavyosimamia uwazi na uwajibikaji katika uteuzi wa umma.
Jaji Mwamuye ameshikilia kwamba mchakato wa uteuzi ulikuwa hauendani utaratibu wa katiba, akiongeza kuwa uchapishaji wa Gazeti hauwezi kuhalalisha mchakato usio halali.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































