ARSENAL WATWAA UBINGWA WA EPL BAADA YA MIAKA 22
Arsenal hatimaye wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi kuu ya Uingereza baada ya kusubiri kwa miaka 22, kufuatia sare ya 1-1 baina ya Manchester City na Bournemouth.
Matokeo hayo yamewafanya Arsenal kuhitimisha msimu wakiwa kileleni, na kukata ukame wa mataji uliodumu kwa miaka sita chini ya kocha Mikel Arteta.
Timu hiyo imekuwa na msimu imara, ikiwa imepoteza mchezo mmoja tu hivi karibuni na kushinda michezo minne mfululizo bila kuruhusu bao, hatua iliyowawezesha kutwaa ubingwa mapema.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































