HARAMBEE STARS KUMENYANA NA AFRIKA KUSINI KUFUZU AFCON 2027
Safari ya kuelekea mashindano ya AFCON 2027 imeanza rasmi baada ya droo ya mechi za kufuzu kufanyika mjini Cairo ambapo Harambee Stars imepangwa Kundi D pamoja na Afrika Kusini, Guinea na Eritrea
Ingawa Kenya tayari imefuzu moja kwa moja kama mwenyeji mwenza pamoja na Uganda na Tanzania, mechi hizo zitakuwa kipimo muhimu cha maandalizi ya timu hiyo.
Kocha Benni McCarthy sasa atakutana na taifa lake la Afrika Kusini katika mechi inayotarajiwa kuvutia wengi kutokana na historia yake akiwa mchezaji nyota wa Bafana Bafana.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































