HUDUMA ZA USAFIRI ZAREJEA BAADA YA MGOMO KUSITISHWA
Ni afueni kwa wasafiri baada ya huduma za usafiri kurejea kote nchini kufuatia kusitishwa kwa mgomo wa kupinga ongezeko la bei ya mafuta.
Magari ya uchukuzi wa umma yalianza tena kubeba abiria kuanzia Jumanne alasiri baada ya serikali na wadau wa sekta ya usafiri kufikia makubaliano ya kuendelea na mazungumzo kwa muda wa siku saba kutafuta suluhisho la mzozo huo.
Wahudumu wa usafiri pia wamekubaliana kutoongeza nauli kwa sasa huku mazungumzo kuhusu bei mpya ya mafuta yakiendelea.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































