#uncategorized

JUNIOR STARLETS KUWAKABILI UGANDA KUTAFUTA TIKETI YA KOMBE LA DUNIA

Junior Starlets watakutana na timu ya akina dada ya Uganda ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17 Ijumaa katika mechi ya mkondo wa kwanza wa mchujo wa kufuzu kombe la Dunia la akina dada wasiozidi miaka 17.

Kocha Mildred Cheche ameendeleza kikosi kilichofanya vizuri dhidi ya Namibia, akifanya mabadiliko machache kutokana na majeraha.

Beki Rose Nangila na Lindey Weey wamekosa mchezo kutokana na majeraha, huku Daisy Adongo na Grace Wangari wakijumuishwa kuimarisha kikosi kuelekea mchezo huo muhimu.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *