#Local News

KINDIKI ASIFIA SEKTA YA USAFIRI KUSITISHA MGOMO

Naibu Rais Kithure Kindiki ameisifu sekta ya usafiri wa umma kwa kuitikia wito wa serikali wa kusitisha mgomo wa kitaifa uliokuwa umepangwa.

Kindiki amesema hatua hiyo imeleta afuweni kwa wananchi waliokuwa wakikabiliwa na changamoto za usafiri katika maeneo mbalimbali nchini.

Aidha, Naibu Rais ameahidi kuwa serikali itaendelea kuchunguza njia zote zinazowezekana ili kupunguza gharama ya mafuta na kupunguza mzigo wa maisha kwa wananchi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *