#Local News

KNEC YAITAKA UMMA KUWA MAKINI KUZUIA KUTAPELIWA

Baraza la Mitihani nchini  (KNEC) limekanusha habari zinazosambaa mitandaoni za kutoa matangazo ya mafunzo bandia  kuhusu tathmini za shule za upili, huku likiwataka  walimu na wanafunzi kuwa makini dhidi ya watapeli wanaotumia jina lake kuwalaghai wananchi 

Kupitia taarifa rasmi, KNEC imesisitiza kuwa haihusiki kwa njia yoyote na mafunzo hayo yanayotangazwa, na kwamba taasisi hiyo haiombi fedha kutoka kwa wadau kwa ajili ya mafunzo ya tathmini, aidha,  imewahimiza wananchi kuthibitisha taarifa zote kupitia njia zake rasmi kabla ya kuchukua hatua yoyote.

Onyo hilo linajiri wakati KNEC inajiandaa kuanza usajili wa wanafunzi wa Gredi ya Kumi kwa tathmini endelevu chini ya mfumo wa elimu wa CBE, na  kuzitaka shule kuhakikisha zinajisajili kama vituo rasmi vya tathmini kabla ya muda uliowekwa kuisha.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *