MALI YAHARIBIWA WAKATI WA MAANDAMANO YA BEI YA MAFUTA
Mali ya thamani isiyojulikana imeharibiwa katika maeneo mbalimbali nchini baada ya wahuni kutumia maandamano ya kupinga ongezeko la bei ya mafuta kuvamia na kupora biashara.
Katika eneo la Naivasha, watu wawili walifariki baada ya polisi kufyatua risasi kwa kundi la watu waliokuwa wakivamia maduka na biashara.
Huko Murang’a, benki na maduka ya jumla yalivunjwa huku wakazi wakieleza matukio hayo kama mashambulizi yaliyopangwa na makundi ya kihalifu yaliyojipenyeza katika maandamano hayo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































