NPS YAPINGA HABARI ZA KUKAMATWA KWA OCS WA NAIROBI CENTRAL
Huduma ya Kitaifa ya Polisi imekosoa taarifa zilizosambaa kuhusu kukamatwa kwa OCS wa Nairobi Central Dishen Ongoya, zikizitaja kama za upotoshaji.
Katika taarifa yake, msemaji wa polisi Muchiri Nyaga amesema madai hayo yaliyosambaa mitandaoni si ya kweli na hayapaswi kuaminika.
Hata hivyo, taarifa hizo zimezua mjadala baada ya ripoti za awali kuashiria kuwa afisa huyo alikuwa amezuiliwa na polisi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































