OMOLLO AKATAA WITO WA KUJIUZULU
Katibu mkuu katika Wizara ya usalama wa ndani Raymond Omollo amekataa wito wa baadhi ya viongozi wa upinzani wanaomtaka ajiuzulu, akisema hakuna msingi wa hatua hiyo.
Akizungumza katika mahojiano na kituo kimoja humu nchini, Omollo amesema madai hayo yanatokana na siasa na si ukweli wa mambo, akisisitiza kuwa anaendelea kutekeleza majukumu yake kikamilifu.
Wito wa kujiuzulu kwake umechochewa na ongezeko la matukio ya vurugu na mashambulizi dhidi ya mikutano ya kisiasa ya upinzani nchini.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































