SERIKALI YATAKA HATUA DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA
Wizara ya Jinsia, Utamaduni na Huduma kwa Watoto imetoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua za haraka kukabiliana na ongezeko la ukatili wa kijinsia na dhuluma dhidi ya watoto nchini.
Waziri Hannah Cheptumo amesema Kenya ilirekodi visa 10,531 vya dhuluma dhidi ya watoto kati ya Januari mwaka jana na Machi mwaka huu.
Amesema serikali na jamii lazima zishirikiane kulinda watoto na kukomesha vitendo vya ukatili.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































