KINDIKI ATAKA UWIANO KATI YA GHARAMA YA MAFUTA NA MAENDELEO
Naibu Rais Kithure Kindiki amewataka Wakenya kuwa na uwiano kati ya matakwa ya kupunguzwa kwa bei ya mafuta na mahitaji ya kuendesha serikali pamoja na kufadhili miradi ya maendeleo.
Akizungumza katika hafla tofauti jijini Nairobi na Machakos Kindiki amesema serikali inaendelea kufanya kazi usiku na mchana kudhibiti gharama ya bidhaa hiyo muhimu.
Kauli hiyo imejiri siku moja baada ya sekta ya usafiri wa umma kusitisha mgomo wake wa siku mbili uliokuwa umeathiri huduma nchini.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































