OKIDI AAMINI MOMBASA UNITED ITASHINDA DERBY
Kocha wa Mombasa United Peter Okidi amesema ana imani kubwa timu yake itaibuka na ushindi dhidi ya Mwatate United katika mechi ya derby itakayochezwa Jumapili katika Uwanja wa Wundanyi.
Okidi amesema ushindi wao wa mabao 2-1 dhidi ya Nairobi City Stars umeongeza morali na kuimarisha mshikamano ndani ya kikosi.
Kocha huyo pia amewataka washambuliaji kutumia vizuri nafasi za kufunga mabao huku akisisitiza nidhamu kwa safu ya ulinzi.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































