RUTO KUANZA ZIARA YA MAENDELEO MKOA WA PWANI
Rais William Ruto amewasili nchini na anatarajiwa kuanza ziara ya siku tano ya maendeleo katika mkoa wa Pwani, akitembelea kaunti sita.
Katika ziara hiyo, serikali inasema Rais atazindua na kukagua miradi mbalimbali pamoja na kukabidhi miradi iliyokamilika kwa wananchi.
Huko Lamu, Ruto anatarajiwa kuzindua soko la samaki la Kizingitini, pamoja na miradi mingine ikiwemo barabara na mradi wa stima katika kaunti za kwale na kilifi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































