RUTO KUREJEA NCHINI LEO
Rais William Ruto anatarajiwa kurejea nchini hii leo huku kukiwa na shinikizo kubwa kutoka kwa wakenya kuhusu swala ya bei ya Mafuta.
Ruto anatarajiwa kufanya mazungumzo na washikadau katika sekta ya uchukuzi kuhusiana na kupunguza bei ya mafuta baada ya sekta hiyo kusitisha mgomo kwa wiki moja ili kufungua njia ya mazungumzo.
Wakenya sasa wanasubiri kusikiza kauli ya Rais kuhusu swala hilo wakati atakapotua kutoka nchini Kazakhstan.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































