SHINIKIZO ZAONGEZEKA KUHUSU MGOMO WA MATATU
Muda wa kusitishwa kwa mgomo wa sekta ya matatu kwa wiki moja unaendelea kuyoyoma huku shinikizo zikiongezeka kwa serikali kutafuta suluhu ya kudumu kabla ya Jumanne ijayo.
Makubaliano ya kusimamisha mgomo huo yalifikiwa kati ya serikali kupitia Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen, Waziri wa kawi Opiyo Wandayi pamoja na wadau wa sekta ya uchukuzi.
Hata hivyo, viongozi wa vyama vya matatu wamesisitiza kuwa hawatakubali chochote isipokuwa serikali ipunguze gharama ya mafuta ambayo wanasema imeathiri pakubwa biashara yao.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































