UEFA YAPANGA MFUMO MPYA WA KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2030
UEFA imetangaza mfumo mpya wa kufuzu kwa kombe la dunia mwaka 2030 utakaoiga mfumo unaotumika katika UEFA Champions League.
Mfumo huo utakuwa na ngazi mbili ambapo mataifa 36 bora yatawekwa katika Ligi ya Kwanza na kugawanywa kwenye makundi matatu yenye timu 12 kila moja.
Timu zitacheza mechi sita dhidi ya wapinzani tofauti, huku mataifa yatakayomaliza juu yakifuzu moja kwa moja kwa Kombe la Dunia na nafasi zilizobaki kuamuliwa kupitia mchujo.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































