#Local News

UPINZANI WATAKA MSWADA WA FEDHA 2026 UKATALIWE

Vyama vya upinzani vya Jubilee na DCP vimewataka Wakenya kuupinga kikamilifu Mswada wa Fedha wa mwaka 2026 wakidai unalenga kurejesha ushuru unaowaumiza wananchi wa kipato cha chini na cha kati.

Viongozi wa vyama hivyo pia wanataka EPRA kuweka wazi mfumo unaotumika kupanga bei ya mafuta nchini huku wakiwasuta viongozi wa sekta ya uchukuzi kwa makubaliano yao na serikali.

Aidha, wameisuta serikali kwa madai ya kutumia kwa siri ushuru wa mafuta kupata faida za kifedha badala ya kusaidia wananchi kukabiliana na gharama ya juu ya mafuta.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *