KINDIKI ATETEA SERIKALI YA RUTO KWA WAKENYA HUKO ELGEYO MARAKWET
Naibu wa Rais Profesa Kithure Kindiki anasema serikali imefanya kila juhudi za kushukisha bei za mafuta ila vita vya izraeli na marekani dhidi ya Iran ndivo vimesababisha kupanda kwa bidhaa hizo.
Akizungumza katika kaunti ya Elgeyo Marakwet,Kindiki anasema serikali inafanya kila iwezavyo kushukisha bei ya bidhaa hivyo na kuhakikisha inashukisha ushuru wake na kutenga fedha za ruzuku.
Kindiki amekashifu viongozi wa upinzani na kuwahusisha pia na maandamano yaliyoshuhudiwa mapema mwezi huu na kukashifu pia uharibifu ambao umeshuhudiwa katika maeneo mengi humu nchini.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































