KRU YAWEKA MKAKATI WA KUIMARISHA RAGA YA WANAWAKE
Mwenyekiti wa chama cha Raga nchini Harriet Okach amesema kuwa kujenga utamaduni imara na endelevu wa rugby ya wanawake ni kipaumbele cha muda mrefu, huku akilenga kuinua mchezo wa wa wachezaji 15s kufikia kiwango cha mafanikio ya Sevens nchini
Amesema mashindano ya Rugby Africa Cup yanayofanyika jijini Nairobi yanatoa nafasi muhimu ya ushindani na maendeleo, yakishirikisha Kenya, mabingwa watetezi Afrika Kusini, Uganda na Madagascar
Okach ameongeza kuwa shirikisho hilo linawekeza katika maendeleo ya ngazi ya chini ikiwemo rugby ya shule na klabu ili kujenga njia wazi ya wachezaji kufika katika timu ya taifa ya Kenya Lionesses
Amesisitiza kuwa uenyeji wa mashindano makubwa nchini ni muhimu katika kuongeza mwonekano wa mchezo wa wanawake pamoja na kuwapa wachezaji wa ndani uzoefu wa ushindani wa kiwango cha juu wakiwa nyumbani.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































