MBIO ZA KUPANDA LIGI KUU ZAPAMBA MOTO NSL
Mbio za kupanda moja kwa moja hadi Ligi Kuu ya FKF zimezidi kupamba moto katika Ligi ya Taifa Daraja la Kwanza huku timu tatu zikifungana kileleni zikiwa zimesalia mechi tano pekee.
3K FC, Migori Youth na Mombasa United zote zina alama 68 baada ya kucheza mechi 33, huku 3K FC wakiongoza kwa tofauti ya mabao.
Kwa kuwa kuna alama 15 pekee zilizosalia kuwania, makosa yoyote katika mechi zilizobaki yanaweza kuamua nani atapanda ligi kuu msimu ujao.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































