#Athletics #Sports

NAIROBI CITY MARATHON YAVUNJA REKODI YA WASHIRIKI

Mashindano ya tano ya Nairobi City Marathon yatakayofanyika Juni 7 yamevutia rekodi ya washiriki 17,000 kutoka nchi 75 duniani, yakionyesha ukuaji mkubwa wa umaarufu wa tukio hilo

Mashindano hayo yatakuwa na vipengele vinne ambavyo ni marathon ya kilomita 42, nusu marathon, mbio za kilomita 10 na 5, zikiwapa fursa wanariadha wa viwango tofauti kushiriki

Mratibu wa mbio Barnaba Korir amesema nafasi zote zilijaa ndani ya wiki tatu tu baada ya usajili kufunguliwa, hali inayoonyesha hamasa kubwa ya kimataifa kwa mashindano hayo yanayoendelea kuiweka Nairobi kwenye ramani ya riadha duniani

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *