NAULI ZAPANDA LICHA YA MAZUNGUMZO
Wasafiri kote nchini wanakabiliwa na gharama kubwa za usafiri baada ya nauli kupanda licha ya wadau wa sekta ya matatu kuahidi kutopandisha bei wakati mazungumzo yanaendelea.
Hapa jijini Nairobi baadhi ya nauli zimeongezeka kwa hadi asilimia 50 kufuatia matamshi ya awali ya waendeshaji wa usafiri wa umma.
Serikali imetakiwa kushughulikia suala la bei ya mafuta huku baadhi ya viongozi wakisema linaongeza gharama ya maisha na kuathiri uchumi pamoja na familia nyingi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































