ORENGO ASEMA MAISHA YAKE YAKO HATARINI
Gavana wa kaunti ya Siaya James Orengo amesema maisha yake yako hatarini baada ya serikali kuondoa walinzi wake bila maelezo.
Akizungumza na kituo kimoja humu nchini, Orengo amesema Inspekta Jenerali wa Polisi anapaswa kuwajibika iwapo jambo lolote litamtokea.
Orengo amesema maafisa wake tisa wa usalama waliokuwa wakimhudumia katika kaunti za Siaya na Nairobi waliondolewa ghafla Jumatano jioni bila sababu kuelekezwa kwake.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































