RUTO KUKUTANA NA WADAU WA SEKTA YA USAFIRI
Rais William Ruto ameanza ziara ya maendeleo ya wiki moja katika eneo la Pwani huku shinikizo likiongezeka la kuzuia mgomo mpya wa kupinga bei ya mafuta.
Ruto aliyerejea nchini kutoka ziara rasmi katika mataifa ya Azerbaijan na Kazakhstan, anatarajiwa kukutana na wadau wa sekta ya usafiri kujadili ongezeko la gharama za mafuta na athari zake kwa uchukuzi.
Wawakilishi wa vyama vya usafiri walitoa makataa ya siku saba kufikia makubaliano na serikali ili kuepusha mgomo mwingine unaoweza kuvuruga huduma za usafiri nchini.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































