#Local News

RUTO KULIHUTUBIA TAIFA HII LEO

Rais William Ruto anatarajiwa kulihutubia taifa wakati wowote kuanzia sasa huku Wakenya wakisubiri kwa hamu kauli yake kuhusu changamoto za kiuchumi zinazoendelea nchini.

Tangazo hilo limetolewa na msemaji wa Ikulu Hussein Mohamed ambaye amesema Rais atazungumza na wananchi lakini hakufafanua ajenda kamili ya hotuba hiyo.

Hotuba hiyo inajiri wakati nchi ikikabiliwa na shinikizo la kupanda kwa bei ya mafuta, changamoto za usafiri pamoja na hofu ya athari za mivutano ya Mashariki ya Kati inayohusisha Iran, Israel na Marekani.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *