#Local News

WANGA A ANDIKA BARUA YA HISIA KWA ORENGO

Gavana wa Kaunti ya Homa Bay Gladys Wanga ameandika barua ya wazi yenye hisia kwa Gavana wa Kaunti ya Siaya James Orengo akisema kauli zake za hivi karibuni zilimuumiza na kumfedhehesha.

Katika taarifa hiyo, Wanga amesema anaongea kama mtu binafsi na si kama Gavana wa Homa Bay wala kama mwenyekiti wa chama cha ODM.

Amesema alikaa kimya mwanzoni akiheshimu uongozi, lakini amesisitiza kuwa baadhi ya kauli zinahitaji kutafakari kwa sababu zinaathiri taswira ya uongozi na heshima ya wanawake serikalini.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *