HATRICK YA LEWANDOWSKI YAWAINUA BARCA
Robert Lewandowski alifunga mara 3 na kuisaidia Barcelona kupata pointi 3 muhimu katika ushindi wao wa mabao 4-2 dhidi ya Celta Vigo, na kupunguza mwanya wa pointi baina ya mabingwa hao na viongozi Real Madrid ambao waliandikisha sare ya kutofungana na Rayo Vallecano.
Kinda Lamine Yamal pia alifunga bao jingine, Marcos Rashford akitoa assists 2 kwenye mchezo huo.
Frenkie de Jong aliondolewa mchezoni baada ya kadi 2 za njano, ila wakati huo tayari pointi 3 zilikuwa kibindoni kwa vijana hao wa Hansi Flick.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































