#Football #Sports

ROSENIOR AONYA CHELSEA KUHUSU NIDHAMU

Kocha wa Chelsea FC, Liam Rosenior, amedai maboresho ya nidhamu kutoka kwa wachezaji wake baada ya Pedro Neto kuwa mchezaji wa tisa wa klabu hiyo kutolewa nje kwa kadi nyekundu msimu huu.

Chelsea walipoteza 2-1 dhidi ya vinara wa Ligi Kuu ya Uingereza, Arsenal FC, katika Uwanja wa Emirates Jumapili, matokeo yanayomaanisha kuwa wameshinda mechi mbili pekee kati ya sita zilizopita katika mashindano yote.

Kwa sasa Chelsea wako nafasi ya sita kwenye jedwali la Ligi Kuu, wakijiandaa kukabiliana na Aston Villa FC walio nafasi ya nne hapo kesho, wakiwa pointi tatu nyuma ya Liverpool FC katika mbio za kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Utovu wa nidhamu umewagharimu sana Chelsea msimu huu, huku Neto akiwa mchezaji wa saba wa klabu hiyo kuonyeshwa kadi nyekundu katika Ligi Kuu pekee. Rosenior ameonya kuwa yuko tayari kuwaweka benchi wachezaji watakaoshindwa kudhibiti hisia zao uwanjani.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

ROSENIOR AONYA CHELSEA KUHUSU NIDHAMU

BUNGE LAFUTILIA MBALI VIKAO VYA LEO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *