#Local News

MWANAMKE AFIKISHWA MAHAKAMANI KUHUSIANA NA KIFO CHA DAKTARI OBWAKA

Mwanamke anayetajwa kuwa mtu wa kuhojiwa kuhusiana na kifo cha daktari bingwa wa wanawake na mkurugenzi wa Hospitali ya Nairobi, Daktari Job Obwaka, amefikishwa katika Mahakama ya Kibera.

Beatrice Wangari alikamatwa Mei 2baada ya kubainika kuwa alikuwa mtu wa mwisho kuonekana na marehemu mwenye umri wa miaka 79 katika Hospitali ya Nairobi.

Daktari Obwaka alitangazwa kufariki alipofikishwa hospitalini baada ya kuugua ghafla akiwa Kitengela mnamo tarehe Moja Mei huku maafisa wa upelelezi wakiomba kumzuilia mshukiwa kwa siku 14 ili kukamilisha uchunguzi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *