TUJU ASALIA MASHAKANI
Mahakama kuu imesitisha ombi la aliyekuwa Waziri wa zamani na katibu mkuu wa chama cha Jubilee Raphael Tuju la kusimamisha mnada wa baadhi ya mali zake zilizopo Karen jijini Nairobi, Mahakama hiyo inasema haiwezi kubatilisha uhamisho wa mali ambao tayari ulikuwa umefanyika kisheria katika mchakato wa kurejesha deni analodaiwa na Benki.
Katika uamuzi huo, Jaji Moses Ado ameeleza kuwa baadhi ya mali hizo tayari zilikuwa zimeuzwa na hivyo mahakama haina uwezo wa kurudisha nyuma shughuli zilizokamilika kwa mujibu wa sheria.
Hata hivyo, mahakama ilimpa Tuju afueni ya muda kwa kuzuia mauzo ya mali nyingine ambazo bado hazijauzwa, kwa masharti kwamba aweke dhamana ya shilingi milioni 50 ndani ya siku 30 huku akisubiri kusikilizwa kwa rufaa yake.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































