MABWAWA YA WAKOLONI YAHIFATHIWA TRANSNZOIA
Serikali ya kaunti ya transnzoia imeanzisha mpango wa kuhifadhi mabwawa 86 ambayo yametelekezwa baada ya kuondoka kwa mkoloni.
Kwa mujibu wa Waziri wa fedha Pepela Wanjala na katibu katika wizara ya maji na mazingira katika kaunti hiyo Dorothy Nyukuri mabwawa hayo yatasaidia kuimarisha maisha ya wakaazi vile vile kuimarisha uchumi katika kaunti hiyo.
Wakaazi wanaoishi karibu na mabwawa hayo wameiomba serikali ya kaunti ya Transnzoia kuwahusisha katika shughuli hiyo kwa manufaa yao wenyewe.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































