AFISA WA POLISI BUNGENI ANACHUNGUZWA KWA KUITISHA HONGO YA SHILINGI ELFU 40
Afisa wa polisi katika Kituo cha Polisi cha Bunge jijini Nairobi anakabiliwa na mashtaka ya ufisadi kwa kujaribu kupora shilingi elfu 40,000 kutoka kwa mshukiwa aliyekuwa na kesi ambayo imechukua muda katika mahakama hiyo bila kutatuliwa
Kulingana na Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC), mshukiwa amekamatwa na polisi na faili yake ikatumwa kwa mKurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) ili kuidhinisha kufunguliwa mashtaka.
Hata hivyo, DPP ameagiza mshukiwa aachiliwe na kesi hiyo kutatuliwa nje ya mahakama
Imetayarishwa na Janice Marete
English 


































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































