BUNGE LAMWIDHINISHA KANJA KUWA INSPEKTA MKUU
Hatimaye bunge la kitaifa limemwidhinisha Douglas Kanja kuwa inspekta mkuu wa polisi, na sasa anasubiri uteuzi rasmi wa Rais William Ruto.
Kanja aliyetueliwa mnamo tarehe 25 mwezi Julai, aidha amepewa mamlaka ya kutoa amri kwa maafisa wa idara ya kitaifa ya polisi.
Kanja alilazimika kuondoka kwenye wadhifa huo aliokuwa akishikilia na kumpisha naibu wake wa kitengo cha polisi wa utawala Gilbert Masengeli ambaye amekuwa kaimu, baada ya kuteuliwa rasmi kwenye wadhifa huo ambao kisheria ulihitaji kupigwa msasa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































