POLISI WANACHUNGUZA MAUAJI KAKAMEGA KUFUATIA KUPATIKANA KWA MWILI BILA KICHWA
Polisi katika Kaunti ya Kakamega wanachunguza kisa cha kutatanisha katika kijiji cha Ebusang’ang’a, eneo la Butsotso ya kati, eneo bunge la Lurambi, ambapo mwili wa mwanamke umepatikana kwenye shamba la mahindi bila kichwa.
Ugunduzi huo wa kutisha umeacha jamii ya eneo hilo katika mshtuko ikidai majibu na hatua za haraka kutoka kwa polisi wa eneo hilo.
Kaka wa mwathiriwa, aliyehuzunishwa na kifo cha dadaye, anasema kwamba alimuona dada yake mara ya mwisho siku ya Jumapili, Oktoba 6.
Mauaji hayo ya kinyama yamezua taharuki kubwa katika kijiji hicho, huku wananchi wakitaka uchunguzi wa haraka kufanywa na polisi la eneo hilo.
Wanajamii wengi wameshutumu mamlaka kwa kushindwa kuwalinda wakitaka maafisa wa polisi katika kituo cha polisi cha eneo hilo wabadilishwe.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































