WAHUDUMU WA UHC WAENDELEZA MGOMO NORTHRIFT

Huduma za matibabu katika vituo mbali mbali vya afya kwenye kaunti zote 7 za Northrift zimeendelea kusambaratika kufuatia mgomo unaoendelea wa wahudumu wa afya walioajiriwa chini ya mpango wa afya kwa wote UHC, ambao wamekongamana mjini Kapsabet kaunti ya Nandi kufanya maandamano. Wahudumu hao wanashinikiza kuajiriwa kwa kanadarasi ya kudumu, wakidai kwamba serikali imewapuuza. Wameapa […]

TULETEE MBOLEA KARIBU, WAKULIMA BUNGOMA

Wakulima wa mahindi katika kaunti ya Bungoma wameitaka serikali kuwasilisha mbolea ya ruzuku katika maeneo ya mashinani ikiwemo kwenye afisi za machifu badala ya maghala ya bodi za nafaka NCPB pekee, wakilalamikia mwendo mrefu wanaotembea kuchukua bidhaa hizo. Wakizungumza na wanahabari katika eneo bunge la Webuye magharibi, wakulima hao wakiongozwa na Nancy Nelima wamesema umbali […]

MGOMO: MATIBABU YALEMAZWA MTRH

Shughuli muhimu za matibabu zimekwama katika hospitali ya rufaa na mafunzo ya Moi jijini Eldoret kutokana na mgomo wa wauguzi ambao umeanza hii leo, wagonjwa wakisalia na mahangaiko. Miongoni mwa malalamishi ya wauguzi hao ni madai kwamba hospitali hiyo imekataa kununua vifaa vya matibabu na hivyo kufanya kazi yao kuwa ngumu. Imetayarishwa na Antony Nyongesa

OLUNGA: WAKENYA WAVUMILIE KOCHA MPYA WA STARS

Nahodha wa Harambee Stars, Michael Olunga, amesema Wakenya wanapaswa kuwa na subira na timu wakati wanajifunza mbinu za kocha mpya. Mshambuliaji huyo anasema Benni McCarthy, aliyeteuliwa hivi karibuni kuwa kocha wa Stars kwa mkataba wa miaka miwili unusu, atakuwa na muda mfupi wa kuandaa kikosi kabla ya mechi ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya […]

NYORO: SIJUI KWANINI NILIFURUSHWA

Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro amesema hajui sababu ya kutimuliwa kwake kutoka wadhifa wa mwenyekiti wa kamati ya bajeti katika bunge la kitaifa, akisisitiza kuwa hajawahi kuzungumziwa na mtu yeyote kutoka mrengo wa Kenya Kwanza kuhusu wadhifa huo. Akizungumza na wanahabari afisini mwake katika majengo ya bunge, Nyoro vile vile amedinda kuzungumzia uhusiano wake na […]

SEKTA YA AFYA YAENDELEA KUATHIRIKA

Masaibu yanayoikabili sekta ya afya yameendelea kuongezeka kutokana na migomo ya mara kwa mara, hii leo viongozi wa muungano wa madaktari KMPDU wakiwaongoza wanachama wake kuandamana jijini Nairobi kuikosoa serikali kutokana na kudorora kwa sekta hiyo. Madaktari hao ambao wameungana na watumishi wengine wa umma, wameandamana kutoka hospitali ya kitaifa ya Kenyatta hadi katika makao […]

UCHUKUZI JOGOO WATATIZWA

Shughuli za uchukuzi zimetatizika kwa muda katika barabara ya Jogoo jijini Nairobi kufuatia maandamano ya wafanyabiashara waliofunga barabara hiyo na kuwasha moto karibu na makutano ya Likoni Road kulalamikia madai ya kuwepo kwa mpango wa kubomoa vibanda vyao. Kulingana na wafanyabiashara hao, hawajapewa eneo mbadala la kuendeleza shughuli zao wakati ambapo vibanda vipya vitakuwa vikijengwa. […]

KENYA MBIONI KUIMARISHA KILIMO

Katika juhudi za kuimarisha utoshelevu wa chakula, serikali ya Kenya imesema iko tayari kushirikiana na serikali ya Uholanzi ili kupiga jeki sekta ya kilimo nchini. Katika kikao na wawekezaji Zaidi ya 50 wa Uholanzi waliomtembelea jijini Nairobi, katibu katika wizara ya biashara na viwanda Juma Mukhwana, amesema baadhi ya juhudi hizo ni ujenzi wa vituo […]

KENYA, UHOLANZI ZASHIRIKIANA

Setkta ya kilimo nchini inatarajiwa kuimarika kufuatia udhabiti wa ushirikiano wa kidiplomasia kati ya Kenya na Uholanzi, mataifa hayo mawili yakitia Saini mikataba kadhaa ya ushirikiano ikiwemo kilimo. Kutiwa Saini kwa mikataba hiyo kumewekwa wazi na Rais William Ruto katika Ikulu ya Nairobi ambako mfalme wa Uholanzi Willem Alexander na mkewe Malikia Maxima wamepokelewa. Kwa […]

WAKULIMA WA NG’OMBE WA MAZIWA KUNUFAIKA NA ONGEZEKO LA MAUZO YA NJE YA NCHI

Wakulima wa ng’ombe wa maziwa watanufaika baada ya Kenya kutangaza mpango wa kuongeza mauzo ya nje ya maziwa hadi KSh bilioni 9 ifikapo 2025, kutoka KSh bilioni 7.3 mwaka 2023. Mwenyekiti wa Bodi ya Maziwa Kenya (KDB), Genesio Mugo, amesema nchi inalenga masoko kama Mashariki ya Kati, Sudani Kusini na Somalia. Serikali inapanga kusindika zaidi […]