WATU 7 WA FAMILIA WAFARIKI KWENYE AJALI HUKO NAIVASHA

Polisi huko Naivasha Kaunti ya Nakuru, wanachunguza ajali ya barabara ambapo watu saba wa familia moja wamefariki.
Ajali hiyo imetokea katika barabara ya Naivasha-Longonot usiku wa kuamkia leo, ikisababisha vifo vya watoto wanne na watu wazima watatu.
Miili ya marehemu imepelekwa katika hifadhi ya maiti ya Naivasha ikisubiri uchunguzi wa maiti.
Imetayarishwa na Janice Marete