MGOMO WA WAUGUZI TAITA TAVETA WANUKIA
Viongozi wa vyama vya wauguzi katika kaunti ya Taita Taveta wametangaza mgomo kuanzia hapo kesho baada ya mazungumzo baina yao na uongozi wa kaunti hiyo kukosa kuzaa matunda.
Viongozi hao ambao walikuwa wametoa ilani ya mgomo wiki jana, wanasema serikali imekosa kuangazia maslahi yao ikiwemo mishahara na ulipaji wa makato yao ya kila mwezi.
Aidha, wamelalamikia kufanya kazi katika mazingira magumu kutokana na ukosefu wa dawa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































