POLOKWANE WAKO MBIONI KUMSAJILI KAHIRO KUTOKA KCB
KLABU ya Polokwane City FC ya Afrika Kusini na vigogo wa Ligi Kuu ya Zambia, Nkana Red Devils, wanaongoza katika mbio za kuwania saini ya mshambuliaji wa KCB FC, Francis Kahiro.
Vilabu vyote viwili vimempa mchezaji huyo mkataba wa miaka miwili lakini bado hajaamua ni wapi anapopendelea.
Mshambulizi huyo alitumia wiki kadhaa nchini Afrika Kusini akifanya majaribio na Polokwane, huku klabu hiyo ikiripotiwa kuvutiwa na uwezo wake wa kupachika mabao.
Iwapo atajiunga na Polokwane, Kahiro ataungana na kipa wa Harambee Stars Brian Bwire.
Iwapo Kahiro atachagua kujiunga na Nkana, atafanya hivyo akitumai kufuata nyayo za Duncan Otieno, Harun Shakava, Duke Abuya ambao walishinda taji la ligi na klabu hiyo mnamo Agosti 2020 na pia na Musa Mohammed ambaye alihamia power dynamos.
Kahiro, ambaye yuko katika kipindi chake cha pili katika klabu ya KCB, alitumia mechi za mkondo wa pili wa msimu wa 2023-2024 huko Bandari na akaichezea Harambee Stars kwa mara ya kwanza Novemba mwaka jana dhidi ya Sudan Kusini.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































