USHAURI WA ARATI KWA GACHAGUA

Gavana wa Kisii ambaye pia ni naibu kinara wa chama cha ODM Simba Arati amemtaka Naibu Rais Rigathi Gachagua kujiepusha na ubabe wa kisiasa na badala yake kuangazia maendeleo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa kituo kikuu cha saratani wakati wa ziara ya Rais William Ruto mjini Kisii, Arati amesisitiza umuhimu wa ushirikiano na umoja katika ustawi wa nchi.
Aidha, gavana huyo amemhimiza Gachagua kudumisha uhusiano wake na Rais Ruto.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa