#Local News

MWANARIADHA REBECCA CHEPTEGEI ALAZWA ICU BAADA YA KUSHAMBULIWA

Mwanariadha wa Uganda Rebecca Cheptegei ambaye alipata majeraha ya moto kwa asilimia 75 baada ya kushambuliwa na anayedaiwa kuwa mpenzi wake amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali moja Eldoret.

Mshukiwa wa shambulio hilo Dickson Ndiema Marangach pia amelazwa katika ICU hiyo hiyo.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo amethibitisha kuwa wawili hao wamelazwa katika chumba cha kuhifadhi maiti ICU lakini anatarajiwa kutoa maelezo mafupi kuhusu hali zao.

Cheptegei alishiriki katika mbio za mita 10,000 katika Olimpiki ya hivi majuzi ya Paris.

Alijeruhiwa vibaya katika shambulio la nyumbani kwake eneo la Kinyoro, Endebes kaunti ya Trans Nzoia Jumatatu asubuhi.

Polisi walisema alivamiwa na mpenzi wake ambaye alimmwagia petroli na kumchoma moto.

Imetayarishwa na Janice Marete

MWANARIADHA REBECCA CHEPTEGEI ALAZWA ICU BAADA YA KUSHAMBULIWA

STARLETS WAINGIA KAMBINI

MWANARIADHA REBECCA CHEPTEGEI ALAZWA ICU BAADA YA KUSHAMBULIWA

MASENGELI AAGIZWA KUJIWASILISHA MAHAKAMANI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *