MSHUKIWA MKUU WA KASHFA YA MAFUTA YA TRITON YA BILIONI 7.6 AKAMATWA
Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) imemkamata mshukiwa mkuu wa kashfa ya Shilingi bilioni 7.6 ya Triton Oil.
Msemaji wa EACC Eric Ngumbi alisema mshukiwa huyo alinaswa kutoka afisi zake jijini Nairobi.
Kwa sasa yuko katika seli katika Mahakama ya Kupambana na Ufisadi ya Milimani akisubiri kufikishwa mahakamani.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































