MIAKA 40 GEREZANI KWA KUMUUA MKEWE NA WATOTO WAKE WANNE

Paul Murage Njuki, mwanaume aliyemuuwa mkewe na watoto wake wanne mnamo Novemba 28, 2021, amehukumiwa kifungo cha miaka 40 gerezani.
Njuki alijisalimisha kwa kituo cha polisi cha Kirinyaga, ambapo amekuwa akizuiliwa kabla ya kupelekwa kwenye Mahakama ya Gichugu.
Mahakama Kuu ya Kerugoya kaunti ya Kirinyaga imemhukumu Njuki baada ya kupatikana na hatia ya kuua familia yake.
Millicent Muthoni na watoto wake wanne wenye umri kati ya mwaka mmoja na miaka 13.
Jaji Richard Mwongo wa Mahakama Kuu ya Kerugoya amesema kuwa mahakama imezingatia ushahidi wote ulioletwa mbele yake, ambao umeonyesha kuwa Murage aliwaua wanafamilia yake.
Mshukiwa amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 40 gerezani, ila ana haki ya kukata rufaa ndani ya siku 14.
Imetayarishwa na Janice Marete